Jumamosi, 01 Dhu al-Qi'dah 1447 | 2026/04/18
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu
kesho kutwa

kesho kutwa

Hizb ut Tahrir / Wilayah Sudan Yahuisha Ibada ya Takbira Katika Mwezi wa Dhul-Hijjah kwa Matembezi ya Kishindo katika Soko Kuu la Port Sudan

Baada ya swala ya Alasiri mnamo siku ya Jumatatu, tarehe 6 Dhul-Hijjah 1446 H, sawia na tarehe 2 Juni 2025 M, Mashababu wa Hizb ut Tahrir / Wilayah Sudan walihuisha ibada ya takbira katika mwezi wa Dhul-Hijjah. Ustadh Muhammad Jami’ (Abu Ayman), Msaidizi wa Msemaji wa Hizb ut Tahrir katika Wilayah ya Sudan, alihutubia waumini katika Msikiti wa Ibn Mas’ud katika soko kuu la Port Sudan baada ya Swalah ya Alasiri, akiwakumbusha juu ya ubora wa siku hizi zilizobarikiwa za Dhul-Hijjah, na jinsi Maswahaba – Mwenyezi Mungu awe radhi nao – walivyozitukuza siku hizi kwa takbira na tahleel. Kisha akaanza kupiga takbira, ikifuatiwa na dua. Baadaye wote wakatoka kwa matembezi ya kishindo wakiwa wamebeba Rayah (bendera) ya Mtume wa Mwenyezi Mungu (saw), na alama kubwa isemayo: "Kuhuisha Ibada ya Takbira katika Mwezi wa Dhul-Hijjah."

Pongezi kwa Idd Al-Adha Iliyobarikiwa 1446 H

Hizb ut Tahrir inatoa pongezi na baraka nyingi zaidi kwa Umma wetu mpendwa wa Kiislamu, wenye subira na wenye kukubali malipo licha ya maafa na majanga yote unaopitia, maafa na majanga ambayo ni mzigo mzito hata kwa kundi lililo imara zaidi la wanadamu, hususan watu wetu wenye subira mjini Gaza na katika Ardhi Iliyobarikiwa ya Palestina, katika Sikukuu ya Idd ul-Adha. Tunamuomba Mwenyezi Mungu azijaalie siku za Idd hii kuwa ni utulivu katika nyoyo zao na wanyanyuliwe daraja mbele ya Mola wa walimwengu wote.

Pongezi kutoka kwa Amiri wa Hizb ut Tahrir, Mwanachuoni mkubwa Sheikh Ata Bin Khalil Abu Al-Rashtah, kwa Waislamu kwa Jumla na Mashababu (wa Hizb ut Tahrir) Hasa katika Sikukuu ya Idd Al-Adha 1446 H sawia na 2025 M

Idd hii inawasili na uvamizi wa Kiyahudi, unaoungwa mkono na Marekani na silaha zake, bado unaendelea dhidi ya Gaza Hashim na Palestina yote. Na watawala katika nchi za Waislamu wanatazama yanayotokea, mbora wao ni yule anayepatanisha kana kwamba yuko kundi lisilofungamana na upande wowote, bali yuko karibu zaidi na Mayahudi. Si ajabu kwamba Marekani, makafiri wakoloni na umbile lao, dola ya Kiyahudi, wanatushambulia. Ni maadui wa Uislamu na Waislamu, sio kuanzia leo bali wa miaka iliyopita.

Jiunge kwa hii RSS feed

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu