Jarida la UQAB Toleo 101 - Juni 2025
- Imepeperushwa katika Jarida la UQAB
- Kuwa wa kwanza kutoa maoni!
Hizb ut Tahrir Wilayah ya Kenya imechapisha toleo jipya la Jarida la UQAB kwa ajili ya mwezi wa Juni 2025 M.
Hizb ut Tahrir Wilayah ya Kenya imechapisha toleo jipya la Jarida la UQAB kwa ajili ya mwezi wa Juni 2025 M.
Shirika la Afya Duniani (WHO) limefichua kuwa takriban wagonjwa 60,000 wa kipindupindu wamerekodiwa nchini Sudan, na kusababisha vifo vya zaidi ya 1640, likionya madhara ya kuporomoka kwa mfumo wa afya nchini humu. Ufichuzi huu unakuja wakati kipindupindu kikienea kwa kasi katika Jimbo la Khartoum, ambapo maambukizi mapya yanazidi 90% ya jumla ya nchi, haswa huko Karari, Omdurman, na Ombada. Mnamo Jumanne, 27/5/2025, Wizara ya Afya ya Sudan ilitangaza kurekodi kesi 2729, pamoja na vifo 172, katika wiki moja. Waziri wa Afya wa Sudan Dkt. Haitham Mohamed Ibrahim alisema kuwa kuenea kwa kipindupindu jijini Khartoum kunatokana na kuzorota kwa hali ya mazingira na matatizo ya vyanzo vya maji ya kunywa. Wakati huo huo, Waziri Mkuu mpya Kamil Idriss anatoa wito kwa WHO, huku ripoti za vyombo vya habari zikisema kuwa anawasiliana na Mkurugenzi Mkuu wa WHO Tedros Adhanom ili kujadili kusaidia juhudi za kudhibiti kipindupindu nchini humu.
Hizb ut Tahrir / Wilayah Sudan, inamuomboleza kwa macho yenye machozi na nyoyo ziliyoridhika na mapenzi ya Mwenyezi Mungu marehemu: Al-Kamel Mohammad Khair
Islamabad, Pakistan – Baraza la mawaziri la Pakistan mnamo Jumanne lilimpandisha cheo Jenerali Syed Asim Munir, mkuu wa jeshi la nchi hiyo, hadi cheo cha field marshal, kufuatia mzozo wa hivi majuzi wa kijeshi kati ya nchi hiyo na India.