Jumapili, 30 Dhu al-Qi'dah 1447 | 2026/05/17
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu
kesho kutwa

kesho kutwa

Umbile la Kiyahudi lina Haki ya Kuwepo na Kujilinda?! Ewe Waziri Mkuu, Ushauri Wetu Pekee - Tafadhali Tubu!

Katika mahojiano na CNN mnamo Novemba 14, 2024, kuhusu kadhia ya Palestina, Waziri Mkuu wa Malaysia Datuk Seri Anwar Ibrahim alikashifu uungaji mkono usioyumba wa Magharibi kwa umbile la Kiyahudi. Ingawa hapo awali alikuwa mwangalifu katika majibu yake, msimamo wa Anwar ulionekana wazi wakati Richard Quest wa CNN alipouliza maswali mawili makuu. Alipoulizwa, “Lakini ungekubali haki ya ‘Israel’ ya kuwepo?” Anwar akajibu, “Ndiyo.” Kwa kujibu lililofuata, “Na haki ya ‘Israel’ ya kujilinda yenyewe?” alijibu vile vile, “Ndiyo.” Majibu haya yasiyo na shaka tangu wakati huo yamezua utata na ukosoaji mkubwa, huku wengi wakihoji kuunganishwa kwao na msimamo wa muda mrefu wa Malaysia kuhusu kadhia ya Palestina.

Pakistan Inahitaji Sheria zinazotokana na Quran Tukufu na Sunnah ya Mtume, na sio Zinazotokana na wingi wa Thuluthi Mbili ya Wabunge

Pakistan inahitaji katiba, sheria na sera zinazotokana na Dini ya watu wake. Hizb ut Tahrir imetayarisha rasimu ya katiba inayotokana na Quran Tukufu na Sunnah. Ibara ya 1 inasema, “Aqeedah ya Kiislamu ndio msingi wa dola. Hii ina maana kwamba kuwepo kwa dola, muundo wake, uwajibikaji wake, na chochote kinachohusiana nayo lazima kiwe na msingi tu juu ya itikadi ya Kiislamu. Vile vile itikadi hii ndio msingi wa katiba na sheria, na hakuna chochote juu yake kitakachoruhusiwa isipokuwa kitokane na Aqida ya Kiislamu.” Hizb ut Tahrir inataja dalili za kina za Kiislamu kwa ibara hii na ibara zote 191 za rasimu ya katiba.

Kadhia ya Palestina ni Kadhia ya Umma wa Kiislamu, sio Jumuiya ya Kimataifa

Mkuu wa Majeshi (COAS), Jenerali Syed Asim Munir, mnamo Ijumaa, tarehe 15 Novemba 2024, alihutubia sherehe maalum ya Mazungumzo ya Margalla 2024 yaliyoandaliwa na Taasisi ya Utafiti wa Sera ya Islamabad (IPRI). COAS ilizungumza juu ya mada ‘Dori ya Pakistan katika Amani na Utulivu.’ Alisema kwamba Pakistan haitakuwa sehemu ya mzozo wowote wa kimataifa. Badala yake Pakistan itaendelea kucheza dori yake kwa amani na utulivu wa kimataifa. Pakistan daima imekuwa ikisisitiza kuanzishwa kwa dola huru ya Palestina.

Kupigana kwa Heshima, au Kutotenda kwa Udhalilifu?!

Mnamo tarehe 30 Oktoba 2024, Naim Qassem alisema katika hotuba yake ya kwanza ya video baada ya kuapishwa kama Katibu Mkuu wa kundi linaloungwa mkono na Iran, “Tofauti kati yetu na ‘Israel’ ni kwamba tunapigana kwa heshima, tukilenga kambi, jeshi, vifaru na askari, huku wao wanaua raia na watu wasio na silaha, na kuangamiza watu na majengo ya miundombinu.”

Jiunge kwa hii RSS feed

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu