Kuweka Matumaini Yenu Kwa Muuaji!
- Imepeperushwa katika Habari na Maoni
- Kuwa wa kwanza kutoa maoni!
- |
Erdogan, ambaye alionekana katika fremu moja na Rais wa Syria Bashar al-Assad katika picha ya familia ya Mkutano wa Kilele wa Jumuiya ya Ushirikiano wa Kiislamu na Umoja wa Kiarabu uliofanyika Riyadh, alijibu maswali ya waandishi wa habari kwenye ndege iliyokuwa ikiregea kutoka ziarani. Erdogan alisema wanataka kuweka mahusiano kati ya Uturuki na Syria kwenye mstari, “Bado nina matumaini kwa Assad, Mungu akipenda, uundaji upya wa sheria kati yetu na Assad utafariji zaidi eneo hilo.”