Mumempindua Dhalimu wa ash-Sham, Basi Msikubali Chochote baada ya Dhalimu huyo Zaidi ya Utawala wa Uislamu na Dola yake, Khilafah
- Imepeperushwa katika Syria
- Kuwa wa kwanza kutoa maoni!
- |
Baada ya miaka kumi na nne ya mihanga mikubwa ya watu wa Syria katika mapinduzi yao yaliyobarikiwa, Damascus ilikuwa kwenye miadi ya ushindi alfajiri ya leo, Jumapili 8 Disemba 2024, kwa Idhini ya Mwenyezi Mungu (swt). Mwenyezi Mungu (swt) alitubariki kwa kupinduliwa kwa dhalimu Assad, baada ya zama za dhulma, uhalifu na udhalimu wa familia ya Assad katika utawala wake wa chuki, wa kimadhehebu kwa muda wa miaka 54. Katika zama zao, walipiga vita Dini, Shariah na waja wa Mwenyezi Mungu (swt). Waliwatia watu kila aina ya mateso. Hakuna ushahidi bora zaidi wa hili kuliko idadi ya kutisha ya wafungwa ambao waliachiliwa huru kutoka kwa magereza yake ya dhulma, maovu.