Ujumbe wa Hizb ut Tahrir Tanzania Wapeleka Risala Maalumu kwa Mufti Mkuu na Baraza Kuu la Waislamu Tanzania (BAKWATA)
- Imepeperushwa katika Tanzania
- Kuwa wa kwanza kutoa maoni!
- |
Mnamo tarehe 6/2/2024, uamuzi ulitolewa na Baraza la Rais mjini Aden kumteua Ahmed Awad bin Mubarak kuwa Waziri Mkuu wa serikali ya Aden, akimrithi Maeen Abdul Malik. Uteuzi wa Ahmed bin Mubarak umekuja baada ya Baraza la Rais kufeli katika maeneo yaliyo chini ya udhibiti wake kuafikiana juu ya idadi ya wagombea wa nafasi ya uwaziri.
Baada ya miaka 12, Rais Erdogan alifanya ziara rasmi nchini Misri na kukutana na Rais wa Misri Sisi. Viongozi hao wawili walitia saini taarifa ya pamoja kuhusu marekebisho ya vikao vya Baraza la Ushirikiano wa Kimkakati wa Ngazi ya Juu.
BBC imeripoti juu ya watu wanaoishi katika eneo lililotengwa la kaskazini mwa Gaza na wameandika kwamba watoto hukosa chakula kwa siku kadhaa. Misafara ya misaada inazidi kunyimwa vibali vya kuingia na umbile la Kiyahudi.
Familia za Mashababu wa Hizb ut Tahrir nchini Jordan, wanaozuiliwa na Mahakama ya Usalama ya Serikali, walifanya walilaani mbele ya Bunge la Wawakilishi, asubuhi ya leo, Jumatano 14/02/2024, ambapo waliitaka Afisi ya Mkuu wa Bunge la Wawakilishi na Mwenyekiti wa Kamati ya Uhuru wa Umma na Haki za Kibinadamu kufanya kazi na kuwasiliana na wale wanaohusika kwa ajili ya kuachiliwa huru mara moja kwa watoto wao waliowekwa kizuizini kwa sababu ya kutoa maoni yao ambapo hawakufanya kitendo chochote cha kigaidi, au uhalifu wowote kwa sheria za usalama wa serikali.
Baada ya mkuu wa ujasusi wa Misri kuwaonya Hamas juu ya ulazima wa kukubali makubaliano ya kubadilishana wafungwa yaliyoandaliwa chini ya mwavuli wa Marekani ndani ya wiki mbili, na kisha tangazo la redio ya jeshi la umbile la Kiyahudi kwamba Misri ingekubali kuivamia Rafah kwa masharti ya kuhakikisha kuwa Wapalestina hawafurushwi hadi Sinai, pia mnamo Jumapili asubuhi, tarehe 11/2/2024, redio hiyo ilinukuu maafisa wa Misri wakiufahamisha upande wa 'Israel' wa kutoupinga uvamizi wa kijeshi wa Rafah katika mji wa Rafah kwa sharti la kuepuka majeruhi ya raia wa Palestina.
Katika matangazo ya moja kwa moja kwenye Chaneli ya Al Jazeera mnamo Jumatatu asubuhi, Februari 12, 2024, msemaji wa Wizara ya Afya, Ashraf al-Qudra, alizungumza na Al Jazeera akielezea uharibifu uliotokea huko Rafah na nyumba zilizolipuliwa, ambazo zilikuwa zinakaliwa na wakaazi na watu waliohamishwa makao yao.
Ifikapo tarehe 28 ya mwezi wa Rajab al-Fard, 1445 H, tutakuwa tumefika mwaka wa 103 wa kuanguka kwa Khilafah ya Uthmaniya... na utapita mwaka mwingine wa Hijria, unaotuleta karibu na kusimamishwa kwa Khilafah Rashida ya pili kwa njia ya Utume.
Kumbukumbu ya kuanguka kwa Khilafah mnamo tarehe 28 Rajab inakuja mwaka huu ikiwa na athari zaidi ya kukumbukwa kuliko miaka iliyotangulia. Inakuja na jeraha la Palestina linalotiririka damu nyingi zaidi kuliko hapo awali, na kutukumbusha kwamba suala la kupotea kwa Palestina lilikuwa na bado lina uhusiano wa karibu na kuanguka kwa Khilafah.
Wakati kama huu mwezi wa Rajab (katika kalenda ya mwandamo wa mwezi) umekaribia tena huku Umma wa Kiislamu ukiwa bado unateseka sana kwa kukosekana Khilafah ya Kiislamu. Hivi sasa miaka mia moja na tatu kamili iliyopita mnamo tarehe 28 Rajab 1342 H, Khilafah ya Kiislamu iliondolewa mikononi mwa dikteta mhalifu, Mustafa Kamal.