Kama Matokeo ya Kutekeleza Kanuni ya Kisekula ya Kibepari, Makampuni ya Hisa Yanaiba Pesa za Wanachi wa Kawaida wa Yemen
- Imepeperushwa katika Yemen
- Kuwa wa kwanza kutoa maoni!
- |
Mnamo siku ya Jumatano, tarehe 18 Dhu al-Qa`adah 1444 H sawia na 07 Juni 2023, Mahakama ya Fedha za Umma katika Manispaa ya Mji mkuu ilitoa uamuzi wake katika kesi ya kile kinachojulikana kama Kampuni ya Sultana Palace, ambapo iliwatuhumu watu 82 kwa kuwalaghai watu 110,000 katika kipindi cha kati ya Januari 2016 na Julai 15, 2020 na tarehe ya baadaye, kupitia hilo, walipata makadirio ya riyal 66,314,405,000.