Alhamisi, 17 Dhu al-Qi'dah 1446 | 2025/05/15
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

Mkataba wa Maelewano na Usaidizi wa Kifedha kwa Jordan Udhibiti Hatari wa Kikoloni wa Marekani

Mnamo siku ya Ijumaa tarehe 16/9/2022, Naibu Waziri Mkuu wa Jordan na Waziri wa Mambo ya Nje na Masuala ya Wageni Ayman Safadi na Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani Anthony Blinken walitia saini, jijini Washington, mkataba mpya wa maelewano kuhusu uhusiano wa kimkakati kati ya nchi hizo mbili kuhusu misaada ya kifedha ambayo Amerika inakusudia kutoa kwa Jordan kwa miaka saba ijayo, ukihakikisha kujitolea kwa Amerika kwa usalama na utulivu wa Ufalme huu.

Soma zaidi...

Chama cha Ushirika wa Kilimo cha Saada nchini Yemen Ukiukaji wa Hukmu za Uislamu na Uhuishaji wa Wazo la Vyama vya Ushirika

Ijapokuwa takriban miezi miwili imepita tangu kuzinduliwa kwa natija nyingi za Chama cha Ushirika wa Kilimo cha Saada, Usajili bado ungali wazi hadi leo kwa kiwango cha elfu kumi kwa kila hisa. Hivyo basi, ni lazima tufafanue uhalisia wa vyama hivyo ambavyo vinakiuka hukmu za Sharia tukufu, na ili kuhakikisha kwamba watu wa Yemen hawaanguki ndani makosa yao hatari.

Soma zaidi...

Mamlaka ya Palestina Inaendelea kutekeleza Dori ya Uvamizi katika Umwagaji damu ya Wapalestina

Kwa kushirikiana na umbile la Kiyahudi na uhali wake, vikosi vya Mamlaka ya kihalifu ya Palestina (PA) huko Nablus, jana usiku, tarehe 9/19/2022, walitekeleza uhalifu wao mbaya wa kumuua kijana Firas Yaish na kuwajeruhi wengine kadhaa, wakati wa uwakandamizaji wao wa waandamanaji wanaopinga kukamatwa kwa Mujahidina Musab Shtayyeh na Brigedia Jenerali Tabila ambao wanatafutwa na umbile la Kiyahudi wakati huo huo vikosi vya uvamizi vilikuwa vikikamata watu katika miji ya Ukingo wa Magharibi, na walowezi walikuwa wakivamia Mji wa Mkongwe wa Hebron wakiwa na ulinzi wa jeshi lao.

Soma zaidi...

Leicester haihusu Ubaniani na Uislamu, lakini inahusu Hindutva na Malengo yake ya Ufashisti kote Ulimwenguni

Machafuko ya hivi majuzi jijini Leicester kwa mara nyingine tena yameangaza mwanga kuhusu itikadi kifashisti ya mrengo wa kulia ya Hindutva. Ghasia za Leicester haziwezi kulaumiwa kwa mvutano kati ya jamii au mechi ya kriketi, kama ambavyo mabadiliko ya tabianchi hayawezi kulaumiwa kwa kutovaa makoti yalitengezwa kwa sufi. Kuna usuli wa masuala haya ambao hauwezi kupuuzwa.

Soma zaidi...

Tusipozisukuma Dola za Kikafiri Katika Mwelekeo Sahihi, Zitatusukuma Katika Mwelekeo wa Makosa!

Katika mkutano na waandishi wa habari mnamo Septemba 14, msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Marekani Ned Price alisema: “Tumeeleza waziwazi kwamba hatuangalii kutambuliwa. Tunaangalia ni wapi - yalipo maslahi yetu, ushirikiano wa kivitendo pekee, ushirikiano wa kivitendo ambao tunatumai utaisukuma Taliban katika mwelekeo sahihi, na tutaendelea kushirikiana nao kwa msingi huo hadi tuone maboresho katika maeneo ambayo tunajali zaidi kuyahusu.”

Soma zaidi...

‘Kujizuilia’ dhidi ya Ujasiri wa Mashambulizi ya Makombora na Mauaji ya Mwezi Mzima kwenye Mpaka wa Bangladesh Yanayofanywa na Dola Dhaifu kama Myanmar Kunathibitisha Udhaifu wa Serikali ya Hasina katika Kulinda Ubwana wa Ummah kutokana na Utiifu kwa

Usiku wa Septemba 9, kombora lililorushwa na jeshi la Myanmar lilimuua kijana wa Rohingya aitwaye Iqbal (17). Mapema siku hiyo hiyo saa sita mchana, mguu wa kijana wa Bangladesh ulilipuliwa na mlipuko wa mgodi katika eneo ‘Lisilo la nchi yoyote’ linalopakana na Tumbru.

Soma zaidi...

Sheria ya Ulinzi kwa Wanaobadili jinsia ni Shambulizi dhidi ya Uislamu na Maadili ya Familia. Watawala wa Pakistan, Ni Watumwa wa Magharibi, Wanaotafuta Kuangamiza Kizazi Chetu Kipya

Mnamo tarehe 5 Septemba 2022, Seneta wa Pakistan Mushtaq Ahmad aliwasilisha mswada wa marekebisho katika Sheria ya Ulinzi kwa Wanaobadili Jinsia kwa Kamati ya Kudumu ya Seneti ya Haki za Kibinadamu. Katika mkutano huo, Seneta Mushtaq Ahmad, alisema kuwa, "‘Transgender’ ni neno la Kimarekani, halina nafasi katika Uislamu, na sheria kuhusu jamii ya watu waliobadili jinsia ni kinyume na Qur'an na Sunnah na itapigia debe ushoga."

Soma zaidi...

“Basi msiwaogope, bali niogopeni Mimi mkiwa nyinyi ni Waumini.”

Waislamu na wasiokuwa Waislamu kwa pamoja walisusia ombi la kutapatapa la kukubaliwa lililoonyeshwa katika msikiti wa katikati mwa London wiki hii. Vyombo vya habari vilialikwa kutazama watoto wa Kiislamu wakilazimishwa kuimba wimbo wa taifa wa Uingereza, ingawa ni maombi ya kumuombe mfalme na ahifadhiwe, atutawale na kuwa washindi juu yetu.

Soma zaidi...

“Blackberry Wakati wa Uvamizi Haina Maana!” Utayari wa Dola ya Khilafah katika Kukabiliana na Maafa na Ajali

Kuporomoka kwa jengo la makaazi katika eneo la Al-Weibdeh katikati mwa mji mkuu, Amman, siku ya Jumanne, kumesababisha vifo vya watu 9 na kujeruhi wengine 10, katika hali isiyokwisha, huku msako wa kuwatafuta manusura ukiendelea kwenye vifusi. Kuna habari ambazo hazijathibitishwa juu ya uwepo wa zaidi ya watu 10 chini ya vifusi, ambao kati yao wako hai, na Manispaa ya Amman imeondoa watu kwenye majengo 4 karibu na jengo lililoporomoka.

Soma zaidi...

Kati ya Kibaraka Msaliti na Mnafiki Mrongo Watawala wa Waislamu Watoa Rambirambi kwa Mvunjaji wa Khilafah, Uingereza, kwa Kifo cha Malkia Wake

Mnamo Novemba 20,1922, katika Kongamano la Lausanne, Waziri wa Mambo ya Nje wa Uingereza George Curzon aliweka masharti manne kwa nchi yake kukubali kuutambuliwa uhuru wa Uturuki, nayo nii: kuondolewa kabisa kwa Khilafah, kufukuzwa khalifa nje ya mipaka, kunyang'anywa pesa zake, na tangazo kwa dola ya kisekula!

Soma zaidi...

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu