Ijumaa, 18 Rabi' al-thani 1447 | 2025/10/10
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

Simama pamoja na Watu Wasioteteleka wa Gaza, Sio na Trump Mwenye Kiburi!

Miaka miwili imepita tangu mauaji ya halaiki yanayofanywa na umbile nyakuzi la Kiyahudi huko Gaza, ambalo liliyafanya ili kuficha kushindwa kukubwa lilikokupata mnamo Oktoba 7, 2023. Miaka miwili ambayo kila siku ilishuhudia mauaji mapya na ukatili usioelezeka, na dunia nzima imeshuhudia ukatili wa Mayahudi wanyakuzi ambao unakinzana na akili. Watoto, watoto wachanga, nyumba, shule, misikiti na hospitali zililengwa. Watawala wa nchi za Kiislamu walikutana mara kwa mara, wakazungumza, wakalaani, na kisha kutawanyika. Kila shutma iliwashajiisha Mayahudi kufanya uvamizi na mauaji makubwa zaidi. Umbile la Kiyahudi lilifikia hatua ya kuzuia kuingia kwa kipande cha mkate au tama la maji ndani ya Gaza kwa miezi mingi mirefu.

Soma zaidi...

Katika Ziara ya Amerika: Yote yako Pamoja – Kufedheheshwa, Kusihi, Uhalali, Makubaliano, na Majukumu Mapya!

Ziara ya Rais Erdoğan wa Uturuki nchini Marekani kushiriki katika mikutano ya Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa ilikuwa mandhari ya kufedhehesha, sio kwake tu bali kwa viongozi wote wa dola pia. Rais mwenye kiburi wa Marekani Donald Trump alitoa hotuba mbele ya Baraza Kuu ambapo alitangaza kwamba “Marekani imebarikiwa kuwa na uchumi imara zaidi, mipaka yenye nguvu zaidi, jeshi lenye nguvu zaidi...” na kwamba ndani ya miezi minane ya utawala wake aliitoza dunia kodi ya ziada ya kiasi cha dolari trilioni 17, na kwamba Marekani iko katika nafasi nzuri huku nchi zengine “zinaenda kuzimu.” Alisema kuwa maamuzi ya Umoja wa Mataifa hayana maana, na kudai kwamba alimaliza vita saba ndani ya miezi saba. Aliitaja tarehe saba ya Oktoba 2023 kama “unyama wa magaidi wa Hamas,” akizingatia kuwa suluhisho liko katika kuachiliwa huru mara moja kwa wafungwa, na kuongeza kuwa dini inayonyanyaswa zaidi duniani ni Ukristo.

Soma zaidi...

Onyo la Tom Barrack kwa Lebanon Dhidi ya “kuregea Bilad Al-Sham”! Kukiri kwa Siri kwa Marekani kwamba Mradi wa Kuunganisha Ummah Kupitia Usimamishaji wa Khilafah ndio Hasimu Pekee wa Kweli wa Mradi wa Marekani katika Kanda hii

Mnamo 12 Julai 2025, katika mahojiano na Arab News, Mjumbe Maalum wa Marekani katika Mashariki ya Kati, Tom Barrack, alizindua mfululizo mpya wa taarifa zinazofichua mradi wa Marekani katika eneo hili na kuthibitisha kina cha mgogoro ambao utawala wa Marekani unakabiliana nao katika kutekeleza mradi wake wa “Mashariki ya Kati Mpya”.

Soma zaidi...

Hotuba ya Rais Erdoğan ya Umoja wa Mataifa: Maneno Yaso Vitendo

Rais Recep Tayyip Erdoğan, katika hotuba yake kwa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa, alielezea kile kinachotokea Gaza kama “mauaji ya halaiki,” alisisitiza kuwa Israel inaua watoto kila siku, na kutoa wito kwa jumuiya ya kimataifa kuchukua hatua. Akisambaza picha kutoka Gaza, Rais Erdoğan alisema: “Hakuna vita mjini Gaza ... Huu ni uvamizi, uhamishaji, ufukuzaji, mauaji ya halaiki na uharibifu wa maisha.”

Soma zaidi...

Mpango wa Trump ni Uvamizi wa Kikatili wa Kijeshi Ambao Unahitaji Haraka Kubadilishwa kwa Watawala Wanaokubaliana na Mpango Wake

Katikati ya miaka miwili ya vita vya mauaji ya halaiki vinavyoendelea mjini Gaza, Rais wa Marekani Donald Trump alitangaza mpango wa kina unaolenga kumaliza vita katika Ukanda wa Gaza na kufikia “amani ya kudumu” katika Mashariki ya Kati. Mpango huu ulitangazwa wakati wa mkutano wa pamoja wa waandishi wa habari uliofanyika mnamo Jumatatu, 29/9/2025, na mhalifu aliyelaaniwa Benjamin Netanyahu katika Ikulu ya White House. Alisema, “Leo tunalifanyia kazi suluhisho la kina kwa kadhia ya Palestina, sio Gaza pekee.” Miongoni mwa mambo muhimu zaidi katika mpango wake ni mpango wa “kuanzisha chombo kipya cha kimataifa cha uangalizi wa Ukanda wa Gaza kinachoitwa Baraza la Amani.” Aliongeza, “Mimi binafsi nitakuwa mwenyekiti wa baraza hili huko Gaza, kwa ushiriki wa Tony Blair.” Alisisitiza kwamba “washirika wetu wa Kiarabu na Waislamu wako tayari kuchukua majukumu yao kwa Gaza,” na kwamba “ufadhili ni muhimu ili kuruhusu mafanikio mjini Gaza, na tutajenga mustakabali salama zaidi kwa wote.”

Soma zaidi...

Hizb ut Tahrir / Wilayah Uturuki: Kuinusuru Gaza, ni Wito wa Umoja kwa Watawala: “Miaka miwili imepita! Hatungojei Maneno, bali Vitendo!”

Kwa kuzingatia mauaji ya kikatili (mauaji ya halaiki) ambayo yamekuwa yakiendelea kwa miaka miwili kamili, yanayofanywa na umbile halifu la Kiyahudi dhidi ya Waislamu wasio na ulinzi katika Ukanda wa Gaza, ambayo hadi sasa yamesababisha kuuwawa shahidi, kujeruhiwa, na kupoteza zaidi ya wanaume na wanawake wa Kiislamu 240,000, Hizb utTahrir/Wilayah Uturuki, iliandaa matembezi makubwa ya halaiki katika mji mkuu wa Ankara na katika mji wa Istanbul na mji wa Şanlıurfa, yenye kichwa: Wito wa Umoja kutoka Viwanjani kwa ajili ya Gaza katika Mwaka Wake wa Pili: “Wito wa Umoja kwa Watawala: Miaka Miwili Imepita! Hatungojei Maneno, Bali Vitendo!”

Soma zaidi...

Mpango wa Trump ni Sumu Hatari, Ukaliaji Kimabavu wa Marekani na Umoja wa Mataifa wa Gaza, na Uhalifu Mkubwa Uliofanywa na Watawala wa Waislamu

Kujisalimisha na kutoa silaha, kuregeshwa kwa mateka na mabaki ya wafu, na uvamizi unaoongozwa na Marekani, inayoongozwa na Trump kwa jina la Baraza la Amani, likisaidiwa na mwenye chuki dhidi ya Uislamu, Tony Blair, na kutekelezwa na tawala za eneo hili – hizi ndizo sifa za mpango mpya wa Trump, ambao aliutangaza. Amewashukuru viongozi wa nchi za Kiarabu na Kiislamu na washirika wake barani Ulaya kwa mwitikio wao wa dhati kwake, na kutangaza kuwa viongozi wa eneo hilo wanashiriki kikamilifu katika mpango huo wa amani.

Soma zaidi...

Musibabaishwe na Mikutano, Fungueni Mipaka

Katika Mkutano wa Kilele wa Jumuiya ya Ushirikiano wa Kiislamu (OIC) na Ligi ya Nchi za Kiarabu uliofanyika jijini Doha, mji mkuu wa Qatar, Rais Erdoğan alisema: “Tunafahamu kuwa Israel haitasimama katika muda mfupi isipokuwa itakabiliwa na hisia kali na vikwazo. Tunafahamu kwamba tunazo mbinu za kuzuia hili.” (Agencies 15.09.2025)

Soma zaidi...
Jiunge kwa hii RSS feed

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu