Ijumaa, 08 Jumada al-thani 1447 | 2025/11/28
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

Hizb ut Tahrir / Denmark: Kisimamo jijini Copenhagen cha Kuinusuru Gaza yenye Izza!

Kwa kuzingatia mauaji ya kikatili (mauaji ya halaiki) ambayo yamekuwa yakiendelea kwa zaidi ya miezi 19, yanayofanywa na umbile halifu la Kiyahudi dhidi ya Waislamu wasio na ulinzi katika Ukanda wa Gaza uliozingirwa, ambayo yamesababisha kuuawa shahidi na kujeruhiwa kwa wanaume na wanawake wa Kiislamu zaidi ya elfu 185 hadi sasa, Hizb ut Tahrir/Denmark iliandaa kisimamo jijini Copenhagen cha kuwanusuru watu wetu mjini Gaza, na Palestina yote inayokaliwa kwa mabavu kuanzia mto wake hadi bahari yake.

Soma zaidi...

Hizb ut Tahrir / Wilayah Lebanon: Matembezi ya Takbir, Tahlil, na Tahmid 1446 H

Hizb ut Tahrir/Wilayah Lebanon iliandaa maandamano ya Takbir, Tahlil, na Tahmid katika mji wa Tripoli, Syria, chini ya kauli mbiu "Tuko Pamoja nawe, ewe Gaza, tukipiga Takbir na Tahmid," kwa mnasaba wa ujio wa siku kumi za kwanza za Dhul-Hijjah 1446 H – 2025 M Idd al-Adha iliyobarikiwa. Matembezi hayo yalihitimishwa kwa dua ya kugusa moyo ya Sheikh Ahmed Al-Shamali.

Soma zaidi...

Ugonjwa wa Kipindupindu Waangamiza Sudan, na Serikali, kwa Uzembe wake, Inaomba Msaada kwa Mashirika ya Kimataifa!

Shirika la Afya Duniani (WHO) limefichua kuwa takriban wagonjwa 60,000 wa kipindupindu wamerekodiwa nchini Sudan, na kusababisha vifo vya zaidi ya 1640, likionya madhara ya kuporomoka kwa mfumo wa afya nchini humu. Ufichuzi huu unakuja wakati kipindupindu kikienea kwa kasi katika Jimbo la Khartoum, ambapo maambukizi mapya yanazidi 90% ya jumla ya nchi, haswa huko Karari, Omdurman, na Ombada. Mnamo Jumanne, 27/5/2025, Wizara ya Afya ya Sudan ilitangaza kurekodi kesi 2729, pamoja na vifo 172, katika wiki moja. Waziri wa Afya wa Sudan Dkt. Haitham Mohamed Ibrahim alisema kuwa kuenea kwa kipindupindu jijini Khartoum kunatokana na kuzorota kwa hali ya mazingira na matatizo ya vyanzo vya maji ya kunywa. Wakati huo huo, Waziri Mkuu mpya Kamil Idriss anatoa wito kwa WHO, huku ripoti za vyombo vya habari zikisema kuwa anawasiliana na Mkurugenzi Mkuu wa WHO Tedros Adhanom ili kujadili kusaidia juhudi za kudhibiti kipindupindu nchini humu.

Soma zaidi...
Jiunge kwa hii RSS feed

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu