Kitengo cha Wanawake cha Hizb ut Tahrir katika Wilayah Tunisia kinazindua kampeni yenye kichwa “Ufisadi wa Elimu Unatokana na Ufisadi wa Serikali, na Marekebisho Yanahitaji Mabadiliko ya Utawala.”
- Imepeperushwa katika Tunisia
- Kuwa wa kwanza kutoa maoni!
- |
Kwa kuzingatia mgogoro mkubwa unaoathiri sekta zote muhimu nchini kutokana na ushawishi mkubwa wa wakoloni wanaodhibiti taasisi zake kuu, kuzorota kwa sekta ya elimu kumekuwa na athari kubwa sana. Kuzorota huku kunaathiri kila mtu nchini Tunisia— kina baba, kina mama, walimu, na wanafunzi vilevile—kutokana na mshikamano wake tata na pande nyingi zinazopishana.