Gazeti la Al-Raya: Vichwa Vikuu vya Toleo 588
- Imepeperushwa katika Al-Rayah
- Kuwa wa kwanza kutoa maoni!
- |
Hizb ut Tahrir / Wilayah Tunisia katika mji wa Hammamet iliandaa kisimamo kwa kichwa “Ramadhan ni Mwezi wa Quran… Na Quran ni Njia Kamili ya Maisha”
Mwezi mtukufu wa Ramadhan unatukumbusha kwamba Uislamu ulikuja tu kubadilisha ulimwengu na kutatua matatizo ya wanadamu kulingana na muongozo wa Mwenyezi Mungu (swt) na kwa ruwaza iliyowasilishwa katika Quran na Sunnah. Tunaposhuhudia dhulma, ukandamizaji, na misiba mingi na matatizo yanayoukumba ulimwengu wa Kiislamu na wanadamu kwa jumla, ni wazi kabisa kwamba tunahitaji sana ruwaza sahihi ya mabadiliko iliyo wasilishwa na Uislamu.
Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir: Kalima ya Kitengo cha Wanawake kwa Mnasaba wa Ujio wa Mwezi wa Ramadhan Uliobarikiwa 1447 H
Ramadhan inakuja mwaka huu huku Ummah ukisimama kwenye njia panda mpya; kwa upande mmoja unageuka kwenye makaa ya hali ya ukoloni na miiba ya usaliti wa watawala, na kwa upande mwingine hali mpya zinazoibuka za kimataifa, haswa migogoro ya kafiri Magharibi ya kikoloni imetoa fursa mpya ambazo, ikiwa zitakamatwa, zingesababisha Ummah wa Kiislamu kuinuka kwa muda mrefu.
Ardhi za Waislamu zinashambuliwa mfululizo na Amerika na mtoto wake, umbile la Kizayuni. Hii inawezaje kuingia akilini, wakati Amerika imetenganishwa na ulimwengu wa Kiislamu na bahari kubwa?!
Waziri Mkuu wa India Narendra Modi amepangwa kufanya ziara ya kikazi nchini Malaysia mnamo Februari 7-8, 2026, na inaripotiwa kwamba anatarajiwa kupokea mapokezi makubwa kutoka kwa serikali na jamii ya Mabaniani nchini Malaysia. Kibaraka huyu wa Amerika mara nyingi hupokea mapokezi ya heshima katika nchi nyingi kote duniani na hupewa tuzo nyingi na nchi anazotembelea, wakiwemo watawala Ruwaibidha wa Waislamu, kiasi kwamba baadhi wako tayari kukita masanamu ili tu kumfurahisha kiongozi huyu mshirikina.