Jarida la Al-Waie: Vichwa Vikuu vya Habari vya Toleo (474, 475, 476)
- Imepeperushwa katika Jarida la Al-Waie
- Kuwa wa kwanza kutoa maoni!
Baada ya kuchunguza mwezi mwandamo wa Shawwal katika usiku huu mtukufu, usiku wa Alhamisi, kuonekana kwa mwezi mwandamo kumethibitishwa kwa kuonekana halali kisharia katika baadhi ya nchi za Waislamu. Kwa hivyo, kesho Alhamisi itakuwa siku ya kwanza ya mwezi wa Shawwal na siku ya kwanza ya Idd al-Fitr iliyobarikiwa.
Usaidizi wa kimaadili, kidiplomasia, na kisiasa pekee hautoshi kukomesha uvamizi wa kikatili! Waislamu wa Kashmir wanahitaji usaidizi wa kijeshi kutoka kwa Vikosi vya Wanajeshi wa Pakistan na mujahidina.
Kwa imani katika qadhaa ya Mwenyezi Mungu na kukubali mapenzi Yake, Afisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir / Wilayah Jordan inaomboleza mmoja wa wanachama wake, mbebaji da’wah ya Uislamu: Ustadh Ibrahim Ismail Arar (Abu Khalil)
Kwa mnasaba wa kumbukumbu ya miaka 105 H (102 M) ya kuvunjwa kwa Dola ya Kiislamu (Khilafah Uthmani) na wakoloni makafiri, wakisaidiwa na wasaliti wa Kiarabu na Kituruki, na kufutwa kwa mfumo wa utawala wa Kiislamu (Khilafah) kutoka kwa Ummah wa Kiislamu, na kugawanyika kwa ardhi za Waislamu kuwa vidola dhaifu vinavyotawaliwa na vibaraka wa wakoloni makafiri, Hizb ut Tahrir / Wilayah Uturuki iliandaa msururu wa semina na mikutano ya wakati mmoja katika maeneo 50 kote nchini Uturuki chini ya kichwa: “Khilafah si Khiyari, bali ni Dharura ya Kidini!”
Amerika na umbile la Kiyahudi walizindua shambulizi kubwa la pamoja dhidi ya Iran siku ya Jumamosi, huku milipuko ikitikisa mji mkuu, Tehran, na miji mingine kadhaa, ikiwemo Qom, Isfahan, Kermanshah, na Karaj. “Rais wa Marekani Donald Trump alitangaza kuanza kwa shambulizi dhidi ya Iran, akisema, “Tumeanza tu operesheni kubwa za mapigano nchini Iran.” Channel 12 ya ‘Israel’ iliripoti kwamba “Israel” ilishambulia shabaha kadhaa za serikali ya Iran.”
Trump Mtawala wa Kiimla na Mtoto wake, Umbile la Kizayuni, Wameanzisha Shambulizi la Kikatili dhidi ya Iran