Enyi Watu! Je, bado mungali na matumaini kwa Watawala na Wanasiasa Watepetevu (Ruwaibidha) wa Sasa?!
- Imepeperushwa katika Bangladesh
- Kuwa wa kwanza kutoa maoni!
- |
Baada ya kuanguka kwa dhalimu Hasina, watu walitarajia Profesa Yunus achukue hatua madhubuti za kukabiliana na udhibiti wa Marekani-Uingereza-India kwa kutumia ushawishi wake wa kimataifa. Angeweza kuunda mjadala huo na mazingira ya kisiasa nchini humo ambayo kwayo watu wangeweza kuunda suluhisho jipya la kisiasa ili kulinda maslahi ya Uislamu, maslahi ya watu na ubwana wa nchi katika Bangladesh mpya. Ijapokuwa idadi kubwa ya wakaazi wa nchi hii ni Waislamu, serikali ya mpito, kuuondoa Uislamu katika masuluhisho ya kisiasa, haijaondoa marufuku iliyowekwa na dhalimu Hasina kwa chama cha kisiasa cha Hizb ut Tahrir kwa kujisalimisha kwa Marekani-India. Pamoja na hayo, kupitia makongamano ya mtandaoni Hizb ut Tahrir imewasilisha muundo wa dola ya Kiislamu, njia ya kuasisi uchumi unaojitegemea na kuwa na jeshi thabiti kwa ajili ya kulinda ubwana wa nchi hii kwa kuzingatia katiba ya Kiislamu ili kutekeleza matumaini na matarajio ya wananchi wa Bangladesh mpya.