Alhamisi, 05 Rajab 1447 | 2025/12/25
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

Mahouthi Wawakamata Mashababu wa Hizb ut Tahrir kwa Kufichua Mkataba wa Trump!

Mnamo Ijumaa, 21/11/2025, kundi la Mahouthi katika Jimbo la Ibb liliwakamata wanachama wawili wa Hizb ut Tahrir, ndugu: Osama Muhammad Mas’ad Al-Wurafi (umri wa miaka 19) na Ibrahim Muhammad Mas’ad Al-Wurafi (umri wa miaka 15) kufuatia usambazaji wao wa toleo lililotolewa na Hizb ut Tahrir lenye kichwa: “Trump Anawaongoza Wafuasi Wake miongoni mwa Watawala katika Ardhi za Waislamu Kwenye Mkataba wa Fedheha na Aibu, Wakiinamisha Vichwa Vyao Nyuma Yake kwa Kuiweka Gaza Hashem chini ya Usimamizi na Ukoloni!” Toleo hili lilisambazwa nchini Yemen na nchi nyingi za Waislamu.

Soma zaidi...

Wanamgambo ni Tishio la Usalama kwa Umbo la Serikali, na Uwepo Wao ni Ukiukaji wa Sharia

Mapigano ya silaha yalitokea katika mji wa Dongola, mji mkuu wa Jimbo la Kaskazini, jioni ya Ijumaa, 21/11/2025, kati ya vikosi vya jeshi la Sudan na kikundi chenye silaha kinachojulikana kama Awlad Gamri, kaskazini mwa kituo cha usafiri wa miji. Kulingana na kile kilichoripotiwa katika habari, kiongozi wa kikundi hicho, anayeitwa Al-Tom Gamri, alijeruhiwa na kupelekwa hospitalini, na kuna habari za kuuawa kwa mlinzi wake binafsi.

Soma zaidi...

Je, Watoto Wafungwa Katika Magereza ya Uvamizi ni Watoto au Wanaume?!

Taasisi za Palestina zinazohusika na masuala ya wafungwa, ikiwemo Klabu ya Wafungwa, zilisema kwamba zaidi ya watoto 1630 kutoka Ukingo wa Magharibi, ikiwa ni pamoja na al-Quds, na makumi kadhaa kutoka Ukanda wa Gaza wamekamatwa na uvamizi tangu mwanzo wa vita dhidi ya Gaza. Waliashiria kuuawa shahidi kwa mtoto mmoja ndani ya Gereza la Megiddo baada ya kukabiliwa na njaa, kunyimwa, na unyanyasaji. 350 kati yao bado wako katika magereza ya uvamizi, wakiwemo wasichana wawili, katika hali ngumu ambazo zinagongana kabisa na viwango vyote vya kimataifa vya ulinzi wa watoto. Wanakabiliwa na uhalifu wa mateso, njaa, na kupuuzwa kimatibabu, vilevile kudhulumiwa kijinsia, pamoja na kutengwa kwa pamoja na kunyimwa kutembelewa.

Soma zaidi...

Uingereza, kupitia Wafuasi wake na Mabwege wake, Imarati na Serikali ya Al-Alimi, Yamezea Mate Aden na Bahari Nyekundu, Lakini Je, Kuna Mtu Yeyote Aliye Tayari Kuifukuza?

Vyombo vya habari ndani na nje ya Yemen vilisambaza, mnamo Jumanne, 18/11/2025, habari za kuwasili kwa Waziri wa Mambo ya Nje wa Uingereza anayeshughulikia Masuala ya Mashariki ya Kati na Afrika Kaskazini, Hamish Falconer, mjini Aden; ambapo alikutana na Rashad Al-Alimi, Mwenyekiti wa Baraza la Rais lenye wanachama wanane, na waziri huyo wa Uingereza pia alikutana na Waziri Mkuu Salem bin Buraik na Waziri wa Mambo ya Nje Dkt. Shaya Zindani, na mawaziri kadhaa, na Mwewe huyo aliandamana na Balozi wa Uingereza mjini Aden, Abda Sharif.

Soma zaidi...

Enyi Watu wa Sudan, Amerika Inaharakisha Kuvuna Matunda ya Vita vyake nchini Sudan, Kwa hivyo Msiiruhusu Itenganishe Darfur

Wakati wa hotuba yake katika Kikao cha Uwekezaji kati ya Marekani na Saudi Arabia, Rais wa Marekani Donald Trump alisema kwamba Mfalme Mtarajiwa Mohammed bin Salman alikuwa ameomba azimio la mgogoro nchini Sudan, akiongeza kwamba alianza kusoma suala hilo nusu saa tu baada ya maelezo ya Mwanafalme huyo. Trump pia aliandika kwenye tovuti yake ya Kijamii ya Truth kwamba atatumia mamlaka ya urais kusimamisha vita mara moja.

Soma zaidi...

Waislamu Maskini Wanastahili Zaidi Uwekezaji wa Watawala Wapumbavu Kuliko Amerika

Mfalme Mtarajiwa wa Saudi Arabia alifanya ziara nchini Marekani mnamo Jumanne, 18/11/2025, ambapo alionyesha kiwango cha upumbavu wake katika kufuja utajiri wa Ummah, kiwango cha utiifu wake kwa bwana wake Amerika, pamoja na kiwango cha usaliti wake kwa Ummah wa Kiislamu, njama yake dhidi yake, na vita vyake dhidi ya Mwenyezi Mungu (swt) na Mtume Wake (saw) kwa kukubali kujiunga na Makubaliano ya Abraham, yaliyowekwa katika usaliti mwingine ambao unahakikisha njia iliyo wazi ya suluhisho la dola mbili.

Soma zaidi...

Gaza Inavuna Mavuno Uchungu ya Baraza la Usalama na Uamuzi wa Baraza la Amani

Siku chache baada ya uamuzi wa Baraza la Usalama, watu wa Gaza walianza kuvuna hasara yake; katika muda usiozidi masaa 24, mashahidi 34—wengi wao wakiwa watoto na wanawake—walikuwa wamepanda daraja hiyo hadi kufikia Alhamisi asubuhi, 20/11/2025, pamoja na makumi ya waliojeruhiwa kutokana na uzito wa njaa na kwenye makucha ya baridi kali. Damu hizi safi zilikuwa maana halisi ya uamuzi ulioipa Amerika usimamizi na mamlaka juu ya Ukanda wa Gaza, ikiruhusu kukata vichwa kama ilivyotaka. Ni uamuzi uliopuuza damu, utajiri, na ardhi za watu wa Palestina katika Ukingo wa Magharibi na kuachilia mkono wa Mayahudi kutumbukia ndani ya damu yetu, ambayo ilienea zaidi ya Gaza hadi Kambi ya Ain al-Hilweh nchini Lebanon.

Soma zaidi...

Trump, Kupitia Azimio la Umoja wa Mataifa na kwa Msaada wa Watawala Waislamu, Anajiandaa Kuiweka Gaza na Eneo la Ash-Sham Chini ya Udhibiti wa Moja kwa Moja wa Kikoloni

Wakati wowote Amerika inaposhindwa kufanya jambo peke yake, hutumia mwavuli dhalimu wa Umoja wa Mataifa. Azimio la kishetani nambari 2803, lililoundwa kukandamiza upinzani wa Palestina, ni hila ya hivi karibuni ya Farauni wa leo, Trump. Kulingana na azimio hili ovu lililopitishwa tarehe 17 Novemba, ambalo serikali ya Pakistan ililipigia kura kwa aibu chini ya amri ya Trump, utawala wa Gaza utawekwa chini ya “Bodi ya Amani (BoP),” inayoongozwa binafsi na Farauni Trump. Azimio hilo hilo lililopitishwa tarehe 17 Novemba linatoa mamlaka kwa “Kikosi cha Kimataifa cha Utulivu,” kinachojumuisha wanajeshi kutoka nchi za Kiislamu, kulinda umbile la Kiyahudi na kupokonya silaha upinzani wa Palestina. Kivitendo, hili litakigeuza kuwa “Kikosi cha Ulinzi cha Israel” kinachofanya kazi chini ya amri ya Trump. “Bodi hii ya Amani (BoP)” na muundo wake wa usalama unaoambatana nayo itasimamia Gaza hadi tarehe 31 Disemba 2027, pamoja na uwezekano wa kuongezwa muda.

Soma zaidi...

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu