Hizb ut Tahrir / Kenya Yafanya Kisimamo cha kutoa Wito wa Amali ya Kijeshi dhidi ya Umbile la Mauaji ya Halaiki la Kiyahudi
- Imepeperushwa katika Kenya
- Kuwa wa kwanza kutoa maoni!
- |
Kufuatia mauaji ya halaiki yanayoendelea kufanywa na umbile la Kiyahudi dhidi ya watu wa Gaza, Hizb ut Tahrir/Kenya mnamo siku ya Ijumaa tarehe 18 Aprili, ilifanya ilifanya kisimamo baada ya Swala ya Jumaa jijini Mombasa na Nairobi. Katika Jiji la Pwani, kisimamo kilifanyika nje ya Masjid Nur huku Nairobi kikifanyika katika Masjid Hidaya mtaa wa Eastleagh. Mada kuu ya Kisimamo ilikuwa ni kuibua wito wa dhati kwa Majeshi katika nchi za Kiislamu kuvunja minyororo ambayo watawala wao wamewaweka katika kambi zao ili wasonge mara moja kuukomboa Msikiti uliobarikiwa wa Al-Aqsa kutoka katika makucha ya Mayahudi wanaoukalia kwa mabavu.