Jumatano, 15 Shawwal 1445 | 2024/04/24
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

KAMPENI YA KUTETEA HAKI ZA WAFUNGWA NA DHIDI YA UTEKAJI NYARA

Kutokana na ukweli kwamba wanaharakati watatu wa Hizb ut Tahrir / Tanzania (Ust. Ramadhan Moshi Kakoso, Wazir Suleiman Mkaliaganda na Omar Salum Bumbo) wanazuiliwa bila ya hukumiwa au ridhaa kwa zaidi ya miaka miwili, dhurufu zizo hizo pia zinawakumba wafungwa wengine miongoni mwa wanachuoni wa Kiislamu wa kundi la Uamsho ambao pia wanazuiliwa kwa zaidi ya miaka saba sasa, pamoja na wafungwa wengineo (Waislamu na wasiokuwa Waislamu) wakinyanyaswa katika hali hiyo hiyo, Hizb ut Tahrir / Tanzania ingependa kutangaza uzinduzi wa kampeni maalumu kutetea haki zao.

Soma zaidi...

KUKAMILIKA KWA KAMPENI YA “UKOMBOZI WA KONSTANTINOPOLI”

Hizb ut Tahrir / Tanzania imekamilisha kampeni ya Ufunguzi wa Konstantinopoli iliyo zinduliwa mwanzoni mwa mwezi huu na Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir, kama kampeni pana ya kiulimwengu kuadhimisha tukio adhimu la Hijria la Ukombozi wa Konstantinopoli (mji wa Heraclius) ambao ulizingirwa kuanzia 26 Rabii' al-Awwal hadi 20 Jumada al-Awwal 857 H sawia na 5 Aprili hadi 29 Mei 1453 M

Soma zaidi...

Pamoja na Kampeni ya Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir Dhidi ya Ukatili wa Uchina kwa Waislamu Eneo la Mashariki Turkestan

Uchina kama taifa la kirasilimali haijihusishi tu kuzitumia kilafi rasilimali za kiasili za mataifa yanayo endelea hususan bara la Afrika na kulazimisha juu yao mzigo wa mikopo usio himilika, pia inatekeleza kampeni ya ghasia, vurugu na ukatili dhidi ya Uislamu na Waislamu wa Turkestan Mashariki, eneo ambalo lilivamiwa kinguvu na kutekwa na Uchina.

Soma zaidi...

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu