Nani Atakayesimama Dhidi ya Mauaji ya Halaiki ya Waislamu Eneo la Turkestan Mashariki?
- Imepeperushwa katika Uchambuzi
- Kuwa wa kwanza kutoa maoni!
- |
Mnamo tarehe 27 Agosti, shirika la habari la ‘Buzzfeed News’ lilichapisha taarifa zilizotokana na uchunguzi ulioegemea maelfu ya picha za satelaiti katika eneo la ‘Xinjiang’ inayofichua “miundo mbinu mikubwa na inayoendelea ya uwekaji kizuizini na kushikiliwa kwa muda mrefu” kwa jamii za Uyghur, Kazakh na Waislamu wengine inayotekelezwa na utawala wa kidhalimu wa China.