Jinsi Viongozi wa Waislamu Wanavyoitelekeza Gaza kwa ajili ya Diplomasia na Miamala
- Imepeperushwa katika Habari na Maoni
- Kuwa wa kwanza kutoa maoni!
- |
Rais wa Indonesia Prabowo Subianto alihimiza kusitishwa kwa mapigano mara moja kati ya 'Israel' na Hamas, na akatoa wito wa kusitishwa kwa mzozo wa 'Israel' na Iran. Akizungumza nchini Singapore na Waziri Mkuu Lawrence Wong, Prabowo alisisitiza haja ya azimio la amani kupitia diplomasia. Alionyesha wasiwasi wake mkubwa juu ya vifo vya raia huko Gaza na kuongezeka kwa mvutano katika Mashariki ya Kati. Zaidi ya hayo, alizungumzia mzozo wa Myanmar, akisisitiza kujitolea kwa ASEAN kwa Makubaliano ya Mambo Tano ya kukomesha vurugu na kukuza mazungumzo jumuishi. Indonesia na Singapore zilikubali kuendelea kuunga mkono ushirikiano wa amani nchini Myanmar na kuzingatia kanuni za ASEAN za uthabiti wa kikanda na juhudi za kibinadamu.