Mauaji Yasiyokwisha ya Wanawake na Watoto wa Gaza Kamwe Hayatamalizika hadi Mlinzi na Ngao ya Ummah, Khilafah, Itakaposimamishwa tena
- Imepeperushwa katika Kitengo cha Wanawake Afisi Kuu ya Habari
- Kuwa wa kwanza kutoa maoni!
- |
Huu ni mwaka ambao umeonyesha kwa mara nyingine tena ugumba wa mfumo wa sasa wa dunia, na serikali zake, Umoja wa Mataifa na kila mahakama na taasisi za kimataifa kuwalinda Waislamu wanaodhulumiwa dhidi ya dhalimu wao. Umbile la Kiyahudi limevuka kila mstari mwekundu, limevunja kila mwiko na limekiuka kila kanuni na sheria ya kibinadamu, lakini hakuna serikali ambayo ina utashi wa kisiasa wa kukomesha mauaji haya yasiyokoma.