Mabadiliko ya Kweli Yanaweza Tu Kuja Kutokana na Mradi Unaotokana na Aqidah ya Ummah. Ni nani Aliye Nao?
- Imepeperushwa katika Afisi Kuu ya Habari
- Kuwa wa kwanza kutoa maoni!
- |
Umma wa Kiislamu umeishi kwa karne moja katika unyonge na udhalilishwaji, mfarakano na mgawanyiko, na utegemezi kwa nchi kubwa. Hii inatokana na matendo ya watawala Ruwabidha (wajinga watepetevu) ambao hawaheshimu udugu au ahadi yoyote, wanachojali tu ni kubakia kwenye viti vyao vibovu (vya utawala), kutekeleza mipango ya nchi za Kikafiri katika ardhi zetu ili kukazanisha udhibiti wao juu yetu na kupora mali zetu. Wamesimama dhidi ya kila mtu anayewapinga au kutokubaliana nao, au kujaribu kuwabadilisha, na kuwaweka chini ya kifungo, mateso, mauaji, na ukiukaji wa matukufu. Bashar al-Assad na utawala wake wa kihalifu sio wa mwisho wao, ambaye uhalifu dhidi ya watu wake ulifichuliwa na matukio ya hivi majuzi nchini Syria, uhalifu ambao ni wa aibu na kuwafukuza wale wenye maumbile yaliyo sawa.