Hongera Ash-Sham na Watu wake kwa Kumpindua Mtawala dhalimu na Utawala wake, Sasa ni Mbele Kuelekea Khilafah Rashida
- Imepeperushwa katika Afisi Kuu ya Habari
- Kuwa wa kwanza kutoa maoni!
- |
Asubuhi ya leo, Jumapili tarehe 8/12/2024 M, na katika siku ya 12 ya operesheni ya “Kuzuia Uvamizi”, wapiganaji waliweza kuingia katika mji mkuu wa Syria, Damascus, na kupindua utawala wa Bashar al-Assad, ambaye Reuters iliripoti - ikiwanukuu maafisa wa Syria – kwamba aliuacha mji mkuu na kuelekea kusikojulikana. Hivyo, wapiganaji wa upinzani waliweza kuikomboa Idlib, Aleppo, Hama, Homs na Damascus, na kuwaachilia maelfu ya wafungwa waliokuwa wakizuiliwa na utawala wa kihalifu katika vyumba vya chini vya jela zake ovu kwa miaka na miongo kadhaa.