Jumapili, 25 Shawwal 1447 | 2026/04/12
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

Ujumbe kutoka Hizb ut Tahrir / Wilayah Sudan Wakutana na Mkuu wa Chama cha Wanasheria katika Jimbo la Bahari Nyekundu

Mnamo Jumatatu, 1 Disemba 2025, ujumbe kutoka Hizb ut Tahrir / Wilayah Sudan, ukiongozwa na Ustadh Nasser Ridha, Mwenyekiti wa Kamati Kuu ya Mawasiliano ya Hizb ut Tahrir katika Wilayah Sudan, akifuatana na Ustadh Abdullah Ismail, Mjumbe wa Kamati Kuu ya Mawasiliano ya Hizb ut Tahrir katika Wilayah Sudan, walimtembelea Dkt. Imad al-Din Muhammad Hamdallah, mkuu wa Chama cha Wanasheria katika Jimbo la Bahari Nyekundu, afisini kwake Port Sudan.

Soma zaidi...

Kauli za Patriarch Bechara Al-Rahi Kuhusu Wakristo katika Eneo Hili Mshikamano wa Kudumu kwa Fahamu ya Marekani na Kimagharibi ya “Walio wachache”, iliyo ngeni kwa Watu wa Eneo Hili na Historia Yao!

Katika mahojiano yake na chaneli ya Lebanon Al-Jadeed katika kipindi cha “Huyu ni Mimi” na mwandishi wa habari Samar Abu Khaleel, kauli za Patriarch Bechara Al-Rahi zinaambatana na ziara ya Papa Leo XIV katika eneo hili, ikiwa ni pamoja na Lebanon, hasa kuhusu suala la kubadilisha utawala wa Syria na kauli yake: “Wakristo wanaondoka Syria leo kwa sababu dola iliyopo ni dola ya Kiislamu! Ingawa haikuwa hivyo wakati wa utawala uliopita...” Na msimamo huu ni uthibitisho wa msimamo uliopita wa Patriarch mwenyewe; ambapo alisema mwaka wa 2011 wakati wa ziara yake nchini Ufaransa chini ya Sarkozy: “Kukiri kwamba makosa na ukiukwaji wa sheria uliotokea nchini Syria hakubatilishi ukweli kwamba Rais Bashar Al-Assad alikuwa ameanza mageuzi, na angepaswa kupewa nafasi”!

Soma zaidi...

Kampeni ya Umbile la Kizayuni katika Ukingo wa Kaskazini Magharibi ni Sehemu ya Mpango wake wa Kuimarisha Makaazi na Kuimarisha Udhibiti wake katika Eneo Hilo. Je, Hakuna Kiongozi Anayeongozwa na Mungu wa Kuikomboa Ardhi Iliyobarikiwa?!

Hawa hapa Mayahudi wakizidi kuwa wakali zaidi katika Ukingo wa Magharibi, wakitangaza “operesheni ya kijeshi” kaskazini mwake, wakibomoa nyumba na kuzigeuza zengine kuwa kambi za kijeshi, wakinyang'anya ardhi, wakikamata kundi la Wapalestina na kuua kundi jengine, wakiharibu mifereji ya maji na kung'oa miti, na operesheni yao ya kijeshi inaenea hadi sehemu iliyobaki ya Ukingo wa Magharibi, katikati yake na kusini yake, na hii inaendana na kile walowezi hao wanachofanya, kwa kuzingatia kutolewa kwa sheria inayowaruhusu kupata mali katika Ukingo wa Magharibi, ambayo ilitanguliwa na kufutiliwa mbali kwa sheria ya kutengwa kaskazini yake.

Soma zaidi...

Mwaliko wa Kuhudhuria Muhadhara wa Kisiasa

Afisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir katika Wilayah Sudan inafuraha kuwaalika wataalamu wa vyombo vya habari, wanasiasa, na wale wote wanaopenda masuala ya umma kuhudhuria na kushiriki katika muhadhara mpya ya Kikao cha Kisiasa, ambao utawasilishwa na Ustadh Ibrahim Mushrif, mwanachama wa Afisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir katika Wilayah Sudan, wenye kichwa: Mzozo wa Kikoloni barani Afrika - Sudan kama Mfano

Soma zaidi...

Kongamano la 2025 la Hizb ut Tahrir / Australia ‘Uislamu: Mabadiliko Ambayo Ulimwengu Inahitaji Sana’ Lahitimishwa kwa Mafanikio Makubwa

Hizb ut Tahrir / Australia ilikamilisha kwa mafanikio Kongamano lake la 2025 katika mazingira mazuri ya tafakari ya dhati na wasiwasi wa kweli kuhusu hali ya wanadamu na mwelekeo wake wa baadaye. Kongamano hilo lilijaa hotuba zenye hisia kali na hadhira iliyotiwa moyo na lilijumuisha ujumbe wa video unaotetemesha moyo kutoka katikati mwa Gaza iliyoharibiwa.

Soma zaidi...

Mahouthi Wawakamata Mashababu wa Hizb ut Tahrir kwa Kufichua Mkataba wa Trump!

Mnamo Ijumaa, 21/11/2025, kundi la Mahouthi katika Jimbo la Ibb liliwakamata wanachama wawili wa Hizb ut Tahrir, ndugu: Osama Muhammad Mas’ad Al-Wurafi (umri wa miaka 19) na Ibrahim Muhammad Mas’ad Al-Wurafi (umri wa miaka 15) kufuatia usambazaji wao wa toleo lililotolewa na Hizb ut Tahrir lenye kichwa: “Trump Anawaongoza Wafuasi Wake miongoni mwa Watawala katika Ardhi za Waislamu Kwenye Mkataba wa Fedheha na Aibu, Wakiinamisha Vichwa Vyao Nyuma Yake kwa Kuiweka Gaza Hashem chini ya Usimamizi na Ukoloni!” Toleo hili lilisambazwa nchini Yemen na nchi nyingi za Waislamu.

Soma zaidi...

Wanamgambo ni Tishio la Usalama kwa Umbo la Serikali, na Uwepo Wao ni Ukiukaji wa Sharia

Mapigano ya silaha yalitokea katika mji wa Dongola, mji mkuu wa Jimbo la Kaskazini, jioni ya Ijumaa, 21/11/2025, kati ya vikosi vya jeshi la Sudan na kikundi chenye silaha kinachojulikana kama Awlad Gamri, kaskazini mwa kituo cha usafiri wa miji. Kulingana na kile kilichoripotiwa katika habari, kiongozi wa kikundi hicho, anayeitwa Al-Tom Gamri, alijeruhiwa na kupelekwa hospitalini, na kuna habari za kuuawa kwa mlinzi wake binafsi.

Soma zaidi...

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu