Uvamizi Mpya wa Hay'at Tahrir al-Sham kwa Wanachama wa Hizb ut Tahrir: Hatua ya Kuelekea Uhalalisha Mahusiano au Kuelekea Kujisalimisha?!
- Imepeperushwa katika Syria
- Kuwa wa kwanza kutoa maoni!
- |
Uvamizi mpya wa Huduma ya Kuu ya Usalama yenye uhusiano na Hay'at Tahrir al-Sham (HTS) kwa wanachama wa Hizb ut Tahrir ulikuja baada ya jina kupendekezwa kwa Ijumaa ya 22/11/2024: “Yeyote Anayelinda Mipaka ya NATO, Kuzuia Ufunguzi wa Vita na Kulinda Mipaka ya Utawala.” Huduma Kuu ya Usalama, baada ya uhamasishaji mkubwa iliyoufanya mnamo Ijumaa usiku, iliteka nyara idadi mpya ya wanachama wa Hizb ut Tahrir, ambao ni wakili Muhammad al-Sharif na Fateh al-Tarmanini kutoka mji wa Tarmanin, pamoja na mwanachama Omar Rahhal kutoka mji wa Kafr Nouran, na ndugu wawili, wanafunzi Bashar Abdul-Hay Samsoum na Ahmad Abdul-Hay Samsoum kutoka mji wa Atarib. Hapo awali, Sheikh Amir Salim, ambaye alihamishwa kutoka Jimbo la Daraa, alitekwa nyara.