Jumamosi, 04 Dhu al-Hijjah 1446 | 2025/05/31
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir: Kitengo cha Wanawake: “Enyi Mujahidina wa Ash-Sham! Wacha iwe kwa Ajili ya Mwenyezi Mungu!

Video hii pia inazungumzia jinsi ushindi na mafanikio ya kweli kwa nchi ya Syria na kwengineko yanaweza kupatikana tu kupitia kuziondolea ardhi zetu mabaki yote ya uingiliaji kati na utawala wa wakoloni - ikiwemo vipengele vyote vya mfumo wao wa kisiasa na imani, na kuikumbatia ruwaza ya kweli ya Kiislamu iliyo huru. Hili linaweza kupatikana tu kwa kutekeleza Sheria na Mfumo wa Mwenyezi Mungu (swt) kwa ukamilifu chini ya kivuli cha Khilafah kwa njia ya Utume.

Soma zaidi...

Hizb ut Tahrir / Wilayah Pakistan: Huku Mwezi wa Ramadhan, Mwezi wa Ushindi, Unapokaribia, Umma na Majeshi yake lazima Yakabiliane na Mfumo wa Kilimwengu wa Kidhalimu wa Marekani!

Ramadhan ni mwezi ambao ndani yake Umma wa Kiislamu ulishinda maadui wengi wenye nguvu. Hebu Waislamu na waregeshe hukmu kwa Kitabu cha Mwenyezi Mungu ﷻ katika mwezi wa Ramadhan, na warudishe ushindi dhidi ya maadui, kwa kumtegemea Mwenyezi Mungu ﷻ.

Soma zaidi...

Ukoloni Mamboleo ndio Unaopelekea Ukosefu wa Umeme Nchini Zambia

Tarehe 1 Februari 2025, Bodi ya Udhibiti wa Nishati ya Zambia (ERB) iliongeza muda wa tozo za umeme za dharura za Shirika la Ugavi wa Umeme la Zambia (ZESCO) kwa miezi mitatu ya ziada, ambayo ni kuanzia Februari 1 hadi Aprili 30, 2025, huku nchi ikiendelea kukabiliwa na tatizo kubwa la upungufu wa umeme.

Soma zaidi...

Enyi Majeshi! Chagueni kati ya Watawala hawa ambao ni Watiifu kwa Trump, na Khalifa Rashid ambaye ataikomboa Gaza na Palestina nzima kupitia Nguvu za Kijeshi!

Mnamo Jumanne 4 Februari 2025, akiwa ameketi ubavuni mwa muuaji wa Gaza, Benjamin Netanyahu, Rais Trump wa Marekani alitangaza, "Marekani itauchukua Ukanda wa Gaza, na tutafanya kazi nayo pia." Tamko la kiburi la Trump kuhusu Gaza ni kofi kwenye uso wa watawala wa Waislamu, ambao wametekeleza kwa utiifu amri ya Marekani, na kuzuia vikosi vya majeshi ya Waislamu kupigana na umbile la Kiyahudi, na hivyo kuruhusu mauaji ya Waislamu nchini Palestina. Watawala wa sasa wa Waislamu, kama wale waliotangulia, wanajifunza kwamba Marekani haiwajali wao, au viti vyao vya khiyana. Marekani itaendelea kuwadhalilisha na kuwashusha hadhi mbele ya dunia na watu wao wenyewe. Kwa hakika, kushiriki katika mfumo wa dunia unaoongozwa na Marekani, na kushikamana na sheria za kimataifa na taasisi za kimataifa, si chochote ila unyenyekevu na utiifu kwa Marekani na rais wake. Hata hivyo watawala hawa hawajali. Hata hivi sasa wanakimbilia kumfurahisha na kumtuliza bwana wao, Amerika, wakijaribu kuwasilisha kwake "mpango wa amani wa Waarabu" wao wenyewe.

Soma zaidi...

Miaka Miwili Iliyopita Baada ya Tetemeko la Ardhi la Februari 6 Bado Mateso Hayana Mwisho

Mnamo Februari 6, 2023, matetemeko makubwa mawili ya ardhi yenye kipimo cha 7.8 na 7.5, yaliyopiga kusini na katikati mwa Uturuki na kaskazini mwa Syria, yaliathiri mikoa 11 na kusababisha uharibifu mkubwa na kupoteza maisha. Takriban watu 54,000 nchini Uturuki na 8,500 nchini Syria walipoteza maisha katika matetemeko haya ya ardhi huku kitovu cha matetemeko hayo kikiwa Kahramanmaraş. Jumla ya waliopoteza maisha ilizidi 62,000, na mamilioni ya watu wakabaki bila makao. Hata hivyo, baadhi ya wataalamu wa huru na rasilimali za ndani zinaonyesha kuwa idadi halisi inaweza kuwa kubwa zaidi.

Soma zaidi...
Jiunge kwa hii RSS feed

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu