Ijumaa, 08 Jumada al-thani 1447 | 2025/11/28
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

Hizb ut Tahrir / Wilayah Tunisia: Matembezi ya Ukombozi: “Kwa Netanyahu na Watumishi wake: Khilafah ni Bishara Njema ya Mtume wetu (saw), ambayo inaunganisha Umma na kuangamiza “Ndoto ya Israel Kubwa.”

Mnamo Ijumaa, 22 Agosti 2025, matembezi makubwa yalifanyika katika mji mkuu, Tunis, kutoka Msikiti wa Al-Fath kufuatia swala ya Ijumaa. Matembezi hayo yaliandaliwa na Hizb ut Tahrir/Wilayah Tunisia chini ya kichwa, “Kwa Netanyahu na Watumishi wake: Khilafah ni Bishara Njema ya Mtume wetu (saw), ambayo inaunganisha Umma na kuangamiza “Ndoto ya Israel Kubwa.”

Soma zaidi...

Ubwana Unaofifia: Mpango Mpya wa Mafuta wa Pakistan, Vita vya Kale na Sera ya AI

Mnamo Julai, Rais Trump wa Amerika alichapisha kwenye jukwaa lake la Ukweli wa Jamii. “Hivi punde tumemaliza mkataba na nchi ya Pakistan, ambapo Pakistan na Marekani zitafanya kazi pamoja katika kuendeleza hifadhi yao kubwa ya mafuta.” Mkataba wa mafuta ni sehemu ya mkataba mpana wa kibiashara kati ya nchi hizo mbili, ambapo Marekani imekubali kupunguza ushuru kwa bidhaa za Pakistan kutoka 29% hadi 19%, huku ikitishia kuweka ushuru wa adhabu kwa India, isipokuwa New Delhi imalize uagizaji mafuta ghafi kutoka Urusi.

Soma zaidi...

Waafghani Baina ya Nyundo ya Siasa za Pakistan na Kinoo cha Agenda ya Kikanda

Tangu mwaka wa 2023, serikali ya Pakistan imezidisha uhamishaji wa wakimbizi wa Afghanistan, hatua inayolenga kuishinikiza serikali ya mpito ya Afghanistan inayoongozwa na Taliban jijini Kabul kuwasilisha kikamilifu matakwa ya Amerika. Mawimbi ya Waafghani kuhamishwa kwenda Pakistan yana mizizi ya kihistoria tangu Jihad dhidi ya Muungano wa Kisovieti katika miaka ya 1980, vita vya wenyewe kwa wenyewe vilivyofuata, na uvamizi wa Marekani na kuikalia kijeshi Afghanistan kuanzia 2001 hadi 2021. Pakistan kihistoria imetoa kina cha kimkakati kwa Waislamu wa Afghanistan, shukran kwa mafungamano ya karibu ya kabila yanayovuka Mstari wa Durand.

Soma zaidi...

Ujumbe kutoka Hizb ut Tahrir / Wilayah Sudan Waitembelea Idara ya Muongozo na Ushauri katika Jimbo la White Nile

Ujumbe kutoka Hizb ut Tahrir / Wilayah Sudan – Mji wa Rabak, White Nile, uliitembelea Idara ya Muongozo na Ushauri mnamo Jumapili, 1 Rabi' al-Awwal 1447 H sawia na tarehe 24 Agosti 2025. Ujumbe huo ulikutana na mkuu wa Sekretarieti katika Jimbo la White Nile, Sheikh Abdul Mubara Mahmoud Al-Mahmoud. Ujumbe huo uliongozwa na Dkt. Ahmed Muhammad Fadl Al-Sayyid, mwanachama wa Hizb ut Tahrir, na alifuatana na Ustadh Faisal Madani, mwanachama wa Hizb ut Tahrir.

Soma zaidi...

Uongozi wa Kiislamu Unapokosekana, Ukandamizaji Hutawala

Marekani kwa mara nyengine tena imefichua hali yake ya kiuadui ya sera yake ya kibeberu ya mambo ya nje kwa kutuma manuari tatu kuelekea pwani ya Venezuela. Washington inahalalisha hatua hiyo kupitia tuhuma za muda mrefu kwamba Venezuela inashiriki katika ulanguzi wa madawa ya kulevya-shtaka ambalo Caracas inakataa vikali kama lisilo na msingi na linalochochewa kisiasa.

Soma zaidi...

Uhuru wa Kweli kwa Indonesia

Sherehe ya miaka 80 ya Siku ya Uhuru wa Indonesia ilichangamshwa na mavazi ya kitamaduni ya kupendeza katika Kasri la Merdeka, Jakarta, Jumapili, Agosti 17, 2025. Waziri wa Afya Budi Gunadi Sadikin alihudhuria akiwa amevalia vazi la Batak, akisema alilichagua kwa sababu ya turathi ya mke wake. Waziri wa Nishati na Rasilimali za Madini Bahlil Lahadalia alivalia vazi la kitamaduni la Solo, akibainisha kuwa hapo awali alikuwa amevaa mavazi ya Papua, Sulawesi, na Maluku. Rais Prabowo Subianto alionekana akiwa amevalia Nusantara yenye rangi ya pembe za ndovu akiwa na peci nyeusi, songket sarong, yenye maua ya yasmini. Watu mashuhuri Raffi Ahmad na Nagita Slavina walivalia mavazi ya Kijava, huku Raffi akiwakumbusha wananchi kuchangia vyema kwa taifa. Mabalozi kutoka nchi marafiki walihudhuria wakiwa wamevalia suti rasmi, huku wananchi wengi pia wakiwa wamevalia mavazi ya kikanda, yakionyesha umoja katika utofauti katika sherehe hizo.

Soma zaidi...

Uislamu ni Ujumbe kwa Wanadamu Wote!

Leo hii, watawala mafisadi na wasio na thamani ambao wamejinyakulia madaraka katika ardhi za Waislamu kwa kujidai kuwa wao ndio viongozi wa Uislamu, wanaonyesha na kujifakharisha juu ya mafanikio ya Waislamu huko nyuma, kuwa ni tunu za kihistoria na kiroho, bila ya kuhusisha amri za Shariah kwao wenyewe na mfumo wao wa utawala. Wanazitumia hisia za Waislamu kwa kuwalaza usingizi na kuzikandamiza hasira zao, ambazo hukimbilia uhuru na kujitahidi kutabikisha Shariah katika maisha yao.

Soma zaidi...
Jiunge kwa hii RSS feed

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu