Uacheni! Hakika ni Uvundo
- Imepeperushwa katika Uchambuzi
- Kuwa wa kwanza kutoa maoni!
- |
Ni muhimu kufahamu maana na uhalisia wa neno “Jahiliyah” ili tuifahamu jamii ya sasa ambayo tunaishi. Ili, hitajio la kurejesha tena Khilafah liwe na umuhimu wa kipekee katika maisha ya Waislamu. Tunapoangalia uhalisia wa jamii ya Makkah yenyewe na Waarabu kwa jumla, tunaona kwamba kulikuwa na baadhi ya makabila yanayo hama hama na kulikuwa na uwepo wa makabila kama Thaqif, Quraish, Shaiban na mengineyo.



