Tunawapa Salamu za Idd ul-Adha
- Imepeperushwa katika Kenya
- Kuwa wa kwanza kutoa maoni!
- |
Wakenya wanapambana na nyakati ngumu zaidi juu ya mapendekezo ya Sheria ya Fedha ya 2023. Mswada wa fedha uliowasilishwa bungeni unaregesha asilimia 16 ya ushuru wa ongezeko la thamani (VAT) kwa bidhaa za petroli pamoja na kuanzisha ushuru wa nyumba wa asilimia 3.
Polisi nchini Kenya wanaendelea na ufukuaji wa makaburi membamba kuitoa miili ya watu wanaoaminika kufa njaa katika eneo la pwani ya nchi. Idadi ya vifo hadi sasa imefikia 89 huku miili zaidi ikitarajiwa kutolewa.
Hizb ut Tahrir / Kenya inapenda kutoa salamu za dhati za Idd ul-Fitr yenye baraka kwa Waislamu nchini Kenya na dunia nzima kwa jumla.
Ujumbe kutoka Hizb ut Tahrir/Kenya ukiongozwa na Ustadh Mahd Ali - Mkuu wa Kamati Kuu ya Mawasiliano ya Hizb ut Tahrir nchini Kenya akifuatana na Ustadh Yusuf Ghasani na Ali Mwangi ambao wote ni wanachama wa Hizb ut Tahrir
Mahakama ya upeo nchini Kenya imeamua kuwa jumuiya ya Wasagaji, Mashoga, Wapenda jinsia mbili, Wanaobadili jinsia (LGBTQ) wana haki ya kujumuika. Uamuzi huo sasa unamaanisha hatua ya kukataa kwa Bodi ya Uratibu ya mashirika yasokuwa ya kiserikali (NGOs) kusajili kikundi hiki ni ukiukaji wa haki za binadamu zinazolinda watu wenye msimamo huu wa kingono.
Kama sehemu ya kumbukumbu ya miaka 102 tokea kuvunjwa kwa Khilafah, Hizb ut-Tahrir Kenya iliweza kuandaa maandamano baridi baada ya swala za Ijumaa mnamo tarehe 17 Februari 2023 M sambamba na tarehe 26 Rajab 1444 H.
Utafiti wa serikali wa hivi karibuni umefichua kusheheni pakubwa mahusiano ya nje ya ndoa ambapo inatajwa kuwa wanaume walioko kwenye ndoa wanatoka nje ya ndoa zao kwa kuwa na wapenzi saba huku wanawake nao wakiwa na wapenzi wawili.
Katika hatua ya kuwapa mikopo wafanya biashara wadogo wadogo ambao wamekuwa wakitaabika kuchukua mikopo katika benki kubwa, serikali imezindua mfuko wa fedha unaojulikana maarufu Hustler Fund ambapo baada tu ya uzinduzi huo takriban Wakenya milioni 17 tayari wamechukua mkopo huo kwa muda tu wa saa moja kwenye siku ya kwanza ya uzinduzi huo.
Huku Kenya ikigubikwa na mrundiko wa deni la jumla ya Sh.10 trilioni, Rais William Ruto awataka wakenya wawe wakilipa ushuru vilivyo. Kulingana na rais serikali inanuia kukusanya Sh.2 trillioni kwa mwaka ujao. Rais amewataka raia wawe na tabia ya kulipa ushuru ipasavyo ili kusaidia serikali kulipa deni lake na kuikomboa kutokana na zigo hili.