Katika Ziara ya Amerika: Yote yako Pamoja – Kufedheheshwa, Kusihi, Uhalali, Makubaliano, na Majukumu Mapya!
- Imepeperushwa katika Uturuki
- Kuwa wa kwanza kutoa maoni!
- |
Ziara ya Rais Erdoğan wa Uturuki nchini Marekani kushiriki katika mikutano ya Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa ilikuwa mandhari ya kufedhehesha, sio kwake tu bali kwa viongozi wote wa dola pia. Rais mwenye kiburi wa Marekani Donald Trump alitoa hotuba mbele ya Baraza Kuu ambapo alitangaza kwamba “Marekani imebarikiwa kuwa na uchumi imara zaidi, mipaka yenye nguvu zaidi, jeshi lenye nguvu zaidi...” na kwamba ndani ya miezi minane ya utawala wake aliitoza dunia kodi ya ziada ya kiasi cha dolari trilioni 17, na kwamba Marekani iko katika nafasi nzuri huku nchi zengine “zinaenda kuzimu.” Alisema kuwa maamuzi ya Umoja wa Mataifa hayana maana, na kudai kwamba alimaliza vita saba ndani ya miezi saba. Aliitaja tarehe saba ya Oktoba 2023 kama “unyama wa magaidi wa Hamas,” akizingatia kuwa suluhisho liko katika kuachiliwa huru mara moja kwa wafungwa, na kuongeza kuwa dini inayonyanyaswa zaidi duniani ni Ukristo.



