Jarida la Al-Waie: Vichwa Vikuu vya Habari vya Toleo (465)
- Imepeperushwa katika Jarida la Al-Waie
- Kuwa wa kwanza kutoa maoni!
Mamia ya Mashababu (wanachama) na wafuasi wa Hizb ut Tahrir katika Wilayah ya Lebanon walishiriki katika kisimamo cha kulaani kilichoitishwa na Hizb, baada ya swala ya Ijumaa mnamo tarehe 25/4/2025, jijini Beirut, mbele ya Msikiti wa Mohammad Al-Amin. Kisimamo hicho kilikuwa na kichwa “Kutoka Beirut hadi Gaza, Kuweni Answari wa Mwenyezi Mungu, Enyi Majeshi ya Umma,” ambapo mabango yalinyanyuliwa yakitaka kuhamasishwa kwa majeshi, kupinduliwa kwa viti vya utawala vya madhalimu, na kunusuriwa kwa Gaza kupitia jihad na silaha.
Hizb ut Tahrir Wilayah ya Kenya imechapisha toleo jipya la Jarida la UQAB kwa ajili ya mwezi wa Mei 2025 M.
Video ya afisa mmoja kijana wa jeshi wa Pakistan akitaka kwenda Gaza imesambaa, na wakati huo huo, video nyingine ya afisa sawia wa Misri imesambaa. Enyi maafisa wa majeshi ya Waislamu! Ikiwa hamuwezi kuleta tama la maji au tembe ya tende mjini Gaza, mutawezaje kumleta afisa aliyebeba bunduki?!
Kwa kuzingatia mauaji ya kikatili (mauaji ya halaiki) ambayo yamekuwa yakiendelea kwa zaidi ya miezi 18, yanayofanywa na umbile halifu la Kiyahudi dhidi ya Waislamu wasio na ulinzi katika Ukanda wa Gaza uliozingirwa, ambayo yamesababisha kuuawa shahidi na kujeruhiwa kwa zaidi ya wanaume na wanawake wa Kiislamu 180,000 hadi sasa, Hizb ut Tahrir / Sweden iliandaa kisimamo mbele ya ubalozi wa Marekani katika mji mkuu, Stockholm, chenye kichwa “Risala kwa Majeshi ya Waislamu!”
Hizb ut Tahrir/Wilayat Uturuki inaandaa kongamano la halaiki lenye kichwa “Kongamano Kubwa la Gaza” jijini Ankara, ambapo suluhisho la kweli na la kudumu la kadhia ya Ardhi Iliyobarikiwa (Palestina) litajadiliwa.
Mnamo tarehe 11 Aprili 2025, Mufti Muhammad Taqi Usmani, jaji wa zamani wa Mahakama ya Shirikisho la Sharia, alisema kwamba jihad dhidi ya “Israel” ni faradhi kwa serikali zote za Waislamu. Hata hivyo, licha ya kutangaza kuwa ni wajibu, uongozi wa kijeshi haukukusanya vikosi vya kijeshi kuinusuru Gaza.
Tarehe 7 Aprili 2025, Rwanda ilifanya kumbukumbu ya miaka 31 ya mauaji ya halaiki ya mwaka 1994. Inakadiriwa kuwa takriban Wanyarwanda milioni moja hususan kutoka kabila la Watutsi waliuawa ndani ya takriban miezi mitatu ya mauaji ya halaiki.